Friday, June 17, 2016
KAULI YA JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM KUJISALIMISHA KATIKA KITUO CHA KATI KABLA JESHI LA POLISI HALIJAANZA KUMSAKA:
DAR ES SALAAM.
SIKU CHACHE BAADA YA SAUTI INAYOSADIKIWA KUWA NI YA ASKOFU MKUU WA KANISA LA UFUFUO NA UZIMA JOSEPHAT GWAJIMA KUSAMBAAA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII JESHI LA POLISI LIMEMTAKA KUJISALIMISHA KATIKA KITUO KIKUU CHA POLISI.
INSERT SIRO.
KWA UPANDE WAKE MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI BWANA CHRISTOPHER OLE SENDEKA AMESEMA HAWAJAFANYA UAMUZI WOWOTE KUHUSIANA NA HILO.
INSERT SENDEKA.
POLISI WAMUWINDA ASKOFU GWAJIMA KWA MASAA 7 BILA MAFANIKIO........NI BAADA YA KUSAMBAA KWA SAUTI INAYOSADIKIKA NI YAKE KWENYE MITANDAO YA KIJAMII AKIMSEMA VIBAYA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE:
Polisi walipiga kambi kwa saa saba kwenye geti la nyumba ya Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, wakitaka kumkamata bila ya mafanikio.
Polisi hao walikuwa kama wageni wa askofu huyo wakisubiri wafunguliwe geti, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:10 jioni walipoamua kuondoka wakitumia gari aina ya Toyota Landcruser lenye namba za kiraia, ambalo kwa muda wote huo lilikuwa limeegeshwa pembeni mwa geti hilo.
Thursday, June 16, 2016
ASKOFU GWAJIMA ATETA NA FAMILIA YAKE YA UFUFUO NA UZIMA JUU YA UONGOZI WA CCM KUMPATA MWENYEKITI.
Askofu Mkuu wa kanisa la Ufufuo Na Uzima Dr. Josephat Gwajima afunguka na kusema maovu, yaliotendwa na Serikali ya awamu ya nne .
Pamoja na hayo Askofu Gwajima amempa ushauri Mh. Magufuli kuhusu sakata/mpango unao-endeshwa na vigogo wakubwa, chini kwa chini wa kumnyima uenyekita wa chama katika chama cha mapinduzi (CCM).
Pamoja na hayo Askofu Gwajima amempa ushauri Mh. Magufuli kuhusu sakata/mpango unao-endeshwa na vigogo wakubwa, chini kwa chini wa kumnyima uenyekita wa chama katika chama cha mapinduzi (CCM).
Kutokana na kauli yake ambayo amesikika akisema lisema kuwa kuna mpango wa baadhi ya viongozi wa chama hicho wanaoendesha kampeni ya kusema kuwa sio lazima uwe raisi na kuwa mwenyekiti wa chama.
SHIRIKISHO LA WANAFUZI VYUO VYA ELIMU YA JUU TANZANIA LAPINGA KAULI ZA GWAJIMA JUU YA VIONGOZI WA CCM
Siku chache baada ya Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima kuwashutumu viongozi wa CCM kwamba wanamipango ya kutomkadhi chama Rais Dk. John Magufuli, Shirikiho la Wanafunzi wa vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), limemshukia na kulaani vikali kauli hiyo kwamba ni yauchochezi.
VIDEO YA KIPINDI MAALUM CHA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AALIPOFUTURISHA IKULU JIJINI DSM 14 JUNE 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasihi Watanzania wote kuungana na Waislamu walio katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kuiombea Tanzania iendelee kuwa nchi ya Amani, Utulivu, Umoja na Mshikamano ili iweze kutimiza malengo yake ya kimaendeleo na kuimarisha ustawi wa jamii.
Subscribe to:
Posts (Atom)





