Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasihi Watanzania wote kuungana na Waislamu walio katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kuiombea Tanzania iendelee kuwa nchi ya Amani, Utulivu, Umoja na Mshikamano ili iweze kutimiza malengo yake ya kimaendeleo na kuimarisha ustawi wa jamii.