Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Amos Makalla
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Arumeru
Msshariki Mhe Joshua Nassari aliyekuwa mmoja wa viongozi na wananchi
waliojitokeza kwa wingi kumpokea alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za
Jumuiya ya Afrika Mashariki utofanyika jijini Arusha.PICHA NA IKULU.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli amewasili Mkoani
Arusha ambako pamoja
na mambo mengine ataongoza Mkutano wa 17 wa kawaida
wa
wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki utakaofanyika Jumatano
tarehe 02 Machi, 2016
Mjini Arusha.
Katika uwanja
wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Rais Magufuli amelakiwa na viongozi
mbalimbali wa vyama vya siasa na serikali pamoja na vikundi vya burudani za
ngoma kabla ya kuelekea Arusha Mjini.
Rais Magufuli
ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayojumuisha nchi za
Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.Kabla ya kuongoza kikao hicho Rais
Magufuli anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na viongozi
wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Tarehe 03
Machi, 2016 Rais Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kenya, wataweka jiwe la msingi
katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Arusha - Holili - Taveta - Voi
inayoziunganisha nchi za Tanzania na Kenya.
Barabara hiyo
ni sehemu ya miradi ya maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayotekelezwa
na nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam
28 Februari 2016
No comments:
Post a Comment