SERIKALI
kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi inatarajia kujenga Vyuo
vya Ufundi (VETA) kwa kila wilaya ili kutoa fursa kwa wananchi wengi hususani
vijana kupata mafunzo mbalimbali ya ufundi yatakayowasaidia kujikwamua kiuchumi
na kujenga taifa.
Akijibu
swali la Mbunge wa Lupa Mhe.Victor Kilasike Mwambalaswa (CCM) kuhusu ujenzi wa
vyuo vya VETA kwa kila Wilaya ambapo Wilaya ya Chunya ni moja kati ya Wilaya
kumi za mwanzo zilizo katika mpango wa ujenzi wa vyuo hivyo wakati wa maswali
na majibu, Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Mhe. Mhandisi Stella
Manyanya amesema Serikali kwa kutambua umuhimu wa kuwa na Chuo Cha VETA sio kwa
wilaya ya Chunya tu bali kwa Wilaya zote nchini, tayari maandalizi ya awali ya
ujenzi wa chuo cha VETA ikiwa ni pamoja na kufanya utambuzi wa stadi
zinazohitajika katika vyuo hivyo.
“
Natoa wito kwa wabunge katika majimbo yao kwa kushirikiana na Halmashauri za
Wilaya zote watafute ardhi kwa kutenga maeneo maalum kwa ajili ya ujenzi wa
vyuo hivi ili hata mipango ya ujenzi ikikamilka ikute eneo lipo tayari kwa
kuanza utekelezaji wake”Alisema Mhe.Manyanya.
Mhe.
Mhandisi Stella Manyanya amesema katika mwaka wa fedha wa 2015/2016 Wizara
yangu kupitia Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeshateua wataalamu
elekezi watakaoshindanishwa kutayarisha andiko la jinsi ya kuifanya kazi ya
kubuni majengo na kupata gharama ya kazi hiyo ili kuanza ujenzi mara moja.
Serikali
kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi kwa kushirikiana na
Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imejipanga kutoa elimu bora ya ufundi
yenye kuleta ufanisi katika maendeleo ya ufundi stadi nchini ili kuwawezesha
wahitimu kupata ujuzi ulio bora kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment