Ally Kisengi wa Halmashauri ya Nanyumbu mkaoni Mtwara,
Abdalla Mfaume wa Halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita, baada ya kubainika wakurugenzi
hao wametenda kosa la
kuwahonga wakaguzi wa fedha kutoka
katika ofisi ya Mkaguzi mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) ili
wapewe hati safi huku
Halmashauri hizi zikiwa na ufisadi .
Pia, Waziri Simbachawene amemsimamisha
kazi mkurugenzi Halmashauri ya Tunduma Mkoani Mbeya
Bi Halima Ajali ili kupisha
uchunguzi kutokana matumizi mabaya ya madaraka.
Hata hivyo Waziri Simbachawane
pia ameziagiza mamlaka husika kuwasimisha kazi watendaji wa ofisi ya mkaguzi wa
Hesabu za Serikali nchini,CAG waliohusika kupokea
rushwa kutoka kwa wakurugenzi hao ili watoe hati safi kwenye Halmashauri hizo huku zikiwa na ubadilifu
wa fedha za Umma.
Akizungumza na
waandishi wa habari mda huu Jijini Dar es Salaam,Waziri Simbachawene amesema
Wakurugenzi hao wamegundulika baada ya uchunguzi
wa kina uliofanywa na wizara yake,
Waziri Simbachawene
ameyataja makosa yao kila mmoja wao ambapo amesema Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Misenyi, Bi Chitundu ametenda
ametanda kosa baada ya kumwagiza mweka hazina wake Majaliwa Bikwato atoe rushwa ya Milioni
tatu kwa maafisa ya (CAG) kwa lengo la kuficha kasoro walizoziabini katika
ukaguzi huo ,
Ambapo Maafisa hao wa CAG waliopeka pesa hizo ni Stevin Buawa,John Elias
pamoja na Kilembi Mkole,
Waziri Simbachawene
amesema Katika Halmashauri ya Nanyumbu ambapo ameidai tarehe 26 Juni 2015 mkurugenzi wake bwana Kasengi pamoja na
mweka hazina Pasco Malowo na mwasibu Emmanuel Mugesa wamlimkabidhi fedha ya
Milioni 3 na laki tano afisa wa CAG ambapo afisa huyo alipokea pesa
hizo kwaniaba ya wenzake kwa lengo la kutoa hati safi,
Sanjari na huyo pia Waziri Simbachawene amesema hata katika Halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita ambapo amedai mwezi Novemba mwaka jana ,
Mkurugenzi wa Halmahsauri hiyo Abdalla Mfaume na mweka hazina wake wamliwapat
ia fedha maafisa wakaguzi wa C AG ambao walipokea rushwa ya milioni 16 ili
wafiche ufisadi walioubaini,
Hata hivyo Simachawene
amesema katika Halmashauri hiyo pia kumegundulika kuwepo na ufisadi mkubwa
ukiwemo malipo ya mishahara hewa pamoja na malipo ya milioni 200 yaliotolewa
pasipo kuwa na Stakabadhi ,
Aidha,Waziri
Simbachawene amesema katika wilaya hiyo ambapo mkaguzi wa mkoa wa Geita alipewa Rushwa kutoka kwa viongozi wa wilaya hiyo ili kuficha ufisadi wa milioni 90
ambazo zilitengwa kwa ajili ya kununulia dawa.
Katika hatua nyingine
Waziri Simbachawene amesema Kwa mamlaka
aliyekuwa nayo amemasiamisha kazi pia mkurugenzi wa Mji wa Tunduma Bi
Halima Ajali baada ya kubainika kutumia vibaya madaraka aliyokuwa nayo.
Amesema Mkurugenzi
huyo alikuwa anawatumia watoto wake kwenye shughuli za Halmashauri huku
akiwalipa pesa pamoja na kuikosesha mapato Halmashauri hiyo yaliyotokana
na Ushuru wa Magari kwenye Mpaka wa
Tunduma,
Vilevile waziri
Simbachawene amemteua Erick Mpunda kukaimu nafasi ya
mkurugenzi huyo ambapo Mapunda kabla ya kuteuliwa kwake hapo alikuwa Mkuu wa
Rasilimali watu wmkoani Mbeya.
Waziri Simbachawene
amemuagiza Katibu kongozi kuwasimamisha watendaji wote ambao walihusika na
rushwa hizo kwenye ofisi ya CAG kwa madai kuwa wapo kwenye Mamlaka yake,
No comments:
Post a Comment