Monday, July 10, 2017

WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEA KITUO CHA AFYA CHA KATORO NA KUJIONEA HALI YA KITUO HICHO

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisalimiana na watumishi wa kitupo cha afya cha mji mdogo wa Katoro.Waziri huyo amefika katika  kituo hicho ili kujionea hali ya kituo hicho ambacho kinahudumia idadi kubwa ya wakazi wa mji huo pamoja na jirani zake licha ya kuwa na changamoto ya watumishi pamoja na miundombinu

KIWANDA CHA MCHINA CHAFUNGIWA KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA

 Katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mb.) akiongea na baadhi ya wananchi wa mtaa wa Mivinjeni Buguruni Sukita Alipowatembelea kufuatia kero ya utiririshwaji wa maji yanayosadikiwa kuwa na  kemikali kutoka katika baadhi ya viwanda maji yanayotumiwa na wakazi wa maeneo hayo kwa kumwagilia bustani za mboga mbonga. Kutoka kulia kwake ni Naibu Meya wa  wa Manispaa ya Ilala Bw. Omary Kumbilamoto, Afisa Mazingira Ilala Bw. Adon Mapunda na Diwani wa kata ya Buguruni Bw. Adam Fugane.

Friday, June 23, 2017

KUTOKA SHIMONI KABLA HUJAFA.

Watanzania wametakiwa kusimama katika zamu na nafasi zao ili waweze kutolewa katika mashimo walikowekwa.
Kauli hiyo imetolewa na mwinjilisti wa kimataifa George banali wakati akihubiri katika viwanja vya wapo mission International vilivyoko mbezi Beach Jogoo jijini Dar es salaam,ambapo alisema kuwa njia pekee ya mtanzania kufanikiwa kutoa katika shimo la mateso ni kumpa Yesu maisha yake.
Aidha alisema kuwa kutokana na watu wengi kuendelea kuteseka na kutaabika njia moja tu ni kumpokea bwana Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako na hautaendeleea kukaa katika shimo.
Inawezekana shilo ulilowekwa ni shimo la mateso magonjwa na shida mbalimbali pamoja na kuonewa na nguvu za giza sasa ni wakati wako wa kufunguliwa na kuwekwa huru katika maisha yako.
Mukutano huo bado unaendelea ambapo waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili wanahudumu kama vile Yes Kwaya,faraja Ntaboba,kikundi cha kusifu na kuabudu cha BCIC na waimbaji wengine wengi.

Thursday, April 27, 2017

TGGA YAZINDUA UPANDAJI MITI 600 KILA MKOA TANZANIA.

 Wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari Mtumba Manispaa ya Dodoma wakiwa na miche ya miti kila mmoja wao kabla ya kuipanda kwenye uzinduzi wa upandaji miti uliofanywa kitaifa na Girl Guides Tanzania mkoani humo. PICHA NA JOHN BANDA;

MIAKA 53 YA MUUNGANO; TUULINDE NA KUIMARISHA, TUPIGE VITA DAWA ZA KULEVYWA NA KUFANYA KAZI KWA BIDII

Kila mtanzania ametakiwa kuhakikisha anafanya jitihada za kuimarisha na kulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa miaka 53 iliyopita. 

Akizungumza leo wakati akihutubia wananchi katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano katika uwanja wa Jamhuri uliopo mjini Dodoma, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alisema kuwa ni muhimu watanzania wakalinda Muungano kwa vile una manufaa kwa nchi zote mbili. 

TANZANIA INAHESHIMU NA KUTAMBUA NAFASI YA MWANAMKE KATIKA UONGOZI

Friday, April 21, 2017

WIZARA YA ARDHI NA MAMLAKA YA MAPATO (TRA) WAENDESHA MAFUNZO YA KODI ZA PANGO YA ARDHI NA MAJENGO KWA WAANDISHI WA HABARI

1
Bw. Dennis Masami Mkuu wa Kitengo cha kodi Wizara ya Ardhi akitoa mada kwa wanahabari kwenye semina kuhusu Kodi za pango ya Ardhi na majengo iliyofanyika wizarani hapo ili kuwajegea uwezo wanahabari katika masuala ya sheria na taratibu za ulipaji wa kodi za pango ya Ardhi na kodi za majengo, Semina hiyo ambayo imeshirikisha pia wataalam wa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA) imefanyika leo jijini Dar es salaam ikishirikisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari pamoja na mitandao ya kijamii.