Showing posts with label mkoani Geita. Show all posts
Showing posts with label mkoani Geita. Show all posts

Saturday, June 11, 2016

MASAUNI AFANYA ZIARA MKOANI GEITA, ATEMBELEA KITUO CHA POLISI KILICHOLALAMIKIWA BUNGENI


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiwasili Kituo cha Polisi Runzewe kilichopo Kata ya Uyovu wilayani Bukombe ambacho Mbunge wa Jimbo hilo, Dotto Biteko aliuliza swali la nyongeza Bungeni hivi karibuni akisema kituo hicho kinahitaji matengenezo makubwa na kumuomba Naibu Waziri huyo kufanya ziara jimboni kwake kujionea kituo hicho. Hata hivyo, Masauni alisema Serikali yake itahakikisha kituo hicho kitakuwa katika hali nzuri.