Showing posts with label Mohamed Mpinga. Show all posts
Showing posts with label Mohamed Mpinga. Show all posts

Tuesday, September 27, 2016

MASAUNI AZINDUA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI, KITAIFA MJINI GEITA

Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akitoa hotuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani alioizindua Kitaifa mjini Geita leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Hatutaki Ajali, Tunataka Kuishi”. Katika hotuba yake, Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Monday, July 04, 2016

MAZISHI YA OMARY MASOUD ALIYEKUWA MFANYAKAZI WA KITUO CHA LUNINGA CHA AZAM TV

 Baadhi ya wafanyakazi wa Azam Media wakiwasili katika Msikiti wa Maamur uliopo Upanga Jijini Dar es Salaam ambapo mwili wa marehemu Omary Masoud uliswaliwa. Marehemu Omary alifariki dunia Julai 2 kwa ajali ya pikipiki katika eneo la Boko. (Picha na Francis Dande)