Thursday, April 27, 2017
MIAKA 53 YA MUUNGANO; TUULINDE NA KUIMARISHA, TUPIGE VITA DAWA ZA KULEVYWA NA KUFANYA KAZI KWA BIDII
Kila mtanzania ametakiwa kuhakikisha anafanya jitihada za kuimarisha na kulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa miaka 53 iliyopita.
Akizungumza leo wakati akihutubia wananchi katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano katika uwanja wa Jamhuri uliopo mjini Dodoma, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alisema kuwa ni muhimu watanzania wakalinda Muungano kwa vile una manufaa kwa nchi zote mbili.
Friday, April 21, 2017
WIZARA YA ARDHI NA MAMLAKA YA MAPATO (TRA) WAENDESHA MAFUNZO YA KODI ZA PANGO YA ARDHI NA MAJENGO KWA WAANDISHI WA HABARI
Bw. Dennis Masami Mkuu wa Kitengo cha kodi Wizara ya Ardhi akitoa mada kwa wanahabari kwenye semina kuhusu Kodi za pango ya Ardhi na majengo iliyofanyika wizarani hapo ili kuwajegea uwezo wanahabari katika masuala ya sheria na taratibu za ulipaji wa kodi za pango ya Ardhi na kodi za majengo, Semina hiyo ambayo imeshirikisha pia wataalam wa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA) imefanyika leo jijini Dar es salaam ikishirikisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari pamoja na mitandao ya kijamii.
Wednesday, April 19, 2017
YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA TISA MKUTANO WA SSBA WA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO APRIL 19, 2017.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao cha nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19, 2017.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Bungeni leo
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Mawaziri kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma, Aprili 19, 2017. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Tekinolojia na Mafunzo ya Ufundi Mhandisi Stella Manyanya, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangalla. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Monday, April 17, 2017
Friday, April 14, 2017
KUSANYIKO LA PASAKA LILILOANDALIWA NA WAPO RADIO 98.1 FM LINAENDELEA KATIKA VIWANJA VYA WAPO REDIO AMBAPO NI IJUMAA KUU NA JUMAMOSI
Mambo yanaendelea katika viwanja hivi vya wapo radio 98.1 fm
Askofu John Rwezaura akifungua Kusanyiko la Pasaka liloandaliwa na Wapo redio FM.
Askofu John Rwezaura akifungua Kusanyiko la Pasaka liloandaliwa na Wapo redio FM.
Monday, April 10, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli leo tarehe 9 Aprili 2017 amesherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa katika Taasisi ya Magonjwa ya Saratani ya Ocean jijini DSM na kutoa wito kwa watanzania kumuunga mkono katika kusaidia watu wenye mahitaji ikiwa ni pamoja na wagonjwa.
Mama Janeth Magufuli amesema ameamua kuwatembelea na kuwafariji wagonjwa hospitalini hapo kwa kutoa msaada huo kwa kuwa yeye alizaliwa katika hospitali hiyo tarehe na mwezi kama wa leo
Aidha ametoa wito kwa wananchi kujenga utamaduni wa kuchunguza afya zao mara kwa mara ili kubaini magonjwa yanayoweza kutibika yakiwa katika hatua za awali.
Mama Janeth Magufuli amewapa pole wagonjwa wote waliolazwa hospitalini hapo na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awaponye haraka ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku.
Pia amewapongeza Madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean road kwa kazi kubwa wanayofanya ya kutibu wagonjwa hao.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amemshukuru mke wa Rais Mama Janeth Magufuli kwa moyo wake wa kujitolea kusaidia wagonjwa hospitali hapo na kuahidi kuendelea kumuunga mkono katika jitihaa zake hizo kama walivyofanya leo.
Nae Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dakta Julius Mwaisalage amemshukuru mke wa Rais Mama Janeth Magufuli kwa moyo wake wa kujitolea kwa kusaidia wagonjwa hospitalini hapo kwa kuwa kitendo hicho kinawatia moyo wao kama wauguzi lakini pia kinarudisha imani kwa wagonjwa na kujiona kuwa hawapo peke yao.
Mama Janeth Magufuli kwa kushirikiana na wanawake wa Wilaya ya Ilala na Temeke wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema wametoa msaada wa vitu mbalimbali kama vile mchele,Maharage,sabuni za kufulia,sabuni za kuogea, maziwa ya unga,Juisi ,taulo za kike, vitenge,kanga, misuli,mafuta ya kujipaka na dawa za meno.
Hafla hiyo pia imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kata ya Kivukoni na Sea View ambazo zipo jirani na hospitali hiyo.
APRIL 09,2017,DR JULIUS MWAISALAGE ...MKURUGENZ...
APRIL 09,2017, CUTS ZA WATU NA JENGO MH MKE WA ...
APRIL 09,2017,ndugu SOPHIA MJEMA..MKUU WA WIALY...
APRIL 09,2017,UU UPSOUND ZA KUOMBEA NA KUTOA MS...
APRIL 09,2017, CUTS ZA KUTOA MSAADA NA KUTEMBEL...
APRIL 09,2017, MH MKE WA RASI MAMA MAGUFULI ASH...
Friday, April 07, 2017
Thursday, April 06, 2017
SERIKALI YAUNGANISHA SHULE 417 KWENYE MTANDAO WA INTANETI – WAZIRI MKUU
*Zimo hospitali za wilaya 74, Ofisi za Halmashauri 123, polisi wilaya 131 na Posta 68
*Asema Serikali haina mzaha na rushwa; *Awataka mabalozi watangaze fursa za utalii, biashara na uwekezaji
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali kwa kushirikiana na kampuni ya Viettel ya Vietnam inatekeleza mradi wa ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano vijijini ambao umefanikisha kuweka miundombinu ya mtandao wa intaneti kwenye shule 417 hapa nchini.
Amesema mradi huo ambao unatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2015-2017, umewezesha pia ofisi za Halmashauri za Wilaya 123, Hospitali za Wilaya 74, Vituo vya Polisi vya Wilaya 131 na Ofisi za Posta 68 kufikiwa na mtandao huo.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Aprili 6, 2017) Bungeni mjini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa ya mapitio ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa mwaka 2016/2017 na mwelekeo wa kazi za Serikali kwa mwaka 2017/2018 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake ukiwemo Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018
Waziri Mkuu amesema katika mwaka 2016/2017, baadhi ya kazi zilizofanyika kwenye sekta ya mawasiliano ni pamoja na ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano; Mradi wa Anuani za Makazi na Postikodi; na kuanzisha huduma ya kituo cha Jamii Centre kitakachorahisisha utoaji wa huduma muhimu katika kituo kimoja. Huduma hizo ni kulipa pensheni, ankara na huduma za kibenki.
“Sekta ya mawasiliano inatekeleza Programu ya Miundombinu ya Kikanda ambayo inahusisha Mradi wa Shule Mtandao (e-school), Mradi wa Video Conference ambao unahusisha ununuzi, usimikaji na ufungaji wa vifaa vya TEHAMA katika mikoa 26 na taasisi za Serikali,” amesema.
Amesema Serikali imekamilisha ujenzi wa kituo cha kuhifadhi taarifa na mifumo ya Serikali (Government Data Centre) ambacho lengo lake ni kuimarisha usalama wa mifumo na taarifa unaoenda sambamba na uhakika wa upatikanaji wa taarifa za Serikali katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku.
Akizungumzia kuhusu ujenzi wa viwanda, Waziri Mkuu amesema Serikali inahamasisha wawekezaji wa ndani na nje kujenga viwanda vidogo, vya kati na vikubwa ili kujenga uchumi wa viwanda, na kwamba inatoa kipaumbele kwenye viwanda vile vinavyotumia malighafi zinazopatikana hapa nchini, vinavyotoa ajira kwa watu wengi na vinavyozalisha bidhaa zenye soko hapa nchini na nje ya nchi.
“Katika kuhakikisha Watanzania wanashiriki kikamilifu kwenye uchumi wa viwanda, Serikali inahamasisha zaidi sekta binafsi ya hapa nchini pamoja na mashirika ya umma kujenga viwanda. Jitihada hizo zimewezesha mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF, PPF, LAPF, GEPF, PSPF na NHIF kuanza kufufua, kuendeleza na kujenga viwanda vipya vipatavyo 27 katika maeneo mbalimbali nchini,” amesisitiza.
Ameyataka mashirika ya umma yahakikishe kwamba mipango yao inaendana na utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa ambao dhima yake ni kujenga uchumi wa viwanda.
Akizungumzia kuhusu juhudi za Serikali kupambana na rushwa, Waziri Mkuu amesema Serikali inapambana na rushwa kwa nguvu zake zote na haina mzaha wala uvumilivu na vitendo vya rushwa.
“Hatua zilizochukuliwa kupambana na rushwa tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani Novemba, 2015 zimetambuliwa na mashirika ya Kimataifa yanayojishughulisha na tafiti kuhusu masuala ya rushwa duniani. Taarifa ya Shirika la Transparency International kwenye utafiti wake kuhusu mtazamo wa rushwa mwaka 2016, imeonesha kuwa viwango vya rushwa vinaendelea kupungua hapa nchini,” amesema.
Akifafanua zaidi, Waziri Mkuu amesema katika mwaka wa fedha 2016/2017, Serikali iliweza kuokoa kiasi cha shilingi bilioni 9.75 kutokana na operesheni zilizofanywa na TAKUKURU,
“TAKUKURU imefanya uchunguzi wa majalada 306 ya tuhuma za rushwa na kupata kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini kuendelea na mashtaka kwa majalada 104. Katika kipindi hicho, TAKUKURU iliendesha kesi 674 zikiwemo kesi mpya 182, ambapo katika kesi 97 watuhumiwa walipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo au kulipa faini. Kesi 407 zinaendelea kusikilizwa mahakamani,” amesema.
Amesema katika mwaka ujao wa fedha, Serikali itaendelea na mapambano dhidi ya rushwa hususan katika eneo la ukusanyaji mapato ya Serikali, kudhibiti matumizi ya fedha za umma, malipo hewa, matumizi mabaya ya fedha za ushirika na kuimarisha ufuatiliaji na ukaguzi wa miradi ya maendeleo.
Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema Serikali imefungua balozi mpya sita katika nchi za Algeria, Israel, Korea Kusini, Sudan, Qatar na Uturuki. Amesema Balozi hizo zina kazi ya kuendeleza juhudi za kuitangaza Tanzania kama nchi yenye vivutio vingi vya utalii na rasilimali zinazoweza kutumika kuvuta uwekezaji kutoka mataifa hayo ikizingatiwa utulivu na amani iliyopo nchini.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
- L. P. 980,
DODOMA,
ALHAMISI, APRILI 4, 2017.
KIKWETE AVUNJA REKODI YA KUSHANGILIWA BUNGENI
VIFIJO , vigeregere na nderemo vimetawala bungeni baada ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kutambulishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Kikwete ambaye alimsindikiza mkewe, alitambulishwa mara baada ya mkewe Salma Kikwete kuapishwa kuwa Mbunge wa Kuteuliwa.
Baadhi ya wabunge walisikika wakisema "tumekumiss tumekumiss" huku wengine wakisema apewe awamu nyingine ya kuongoza.
Wengine walitaka Kikwete aruhusiwe kuwahutubia jambo ambalo lilishindikana kwa wakati huo kutokana na sababu za kikanuni, ambapo kabla ya kuruhusiwa kuhutubiwa ilitakiwa kanuni zitenguliwe kwanza.
Spika Ndugai alijaribu kuwatuliza wabunge lakini ilishindikana waliendelea kushangilia huku wakiimba wimbo mpya wa Nay wa Mitego wa 'Wapo'.
Spika Ndugai alichagiza kwa kusema, katika historia ya Bunge haijawahi tokea mgeni akashangiliwa kama ilivyotokea kwa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete na kwamba hii imevunja rekodi.
Baada ya muda Spika aliwasihi wabunge kunyamaza ili shughuli za bunge ziendelee.
Kikwete akiwa na wasaidizi wake pamoja na mwanawe Ali waliondoka kupisha shughuli za Bunge ziendelee kwani angeendelea kuwemo bungeni utulivu ungeendelea kutoweka.HABARI NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Subscribe to:
Posts (Atom)