Thursday, April 06, 2017

KIKWETE AVUNJA REKODI YA KUSHANGILIWA BUNGENI



VIFIJO , vigeregere na nderemo vimetawala bungeni baada ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kutambulishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Kikwete ambaye alimsindikiza mkewe,  alitambulishwa mara baada ya mkewe Salma Kikwete kuapishwa kuwa Mbunge wa Kuteuliwa.

Baadhi ya wabunge walisikika wakisema "tumekumiss tumekumiss" huku wengine wakisema apewe awamu nyingine ya kuongoza.

Wengine walitaka Kikwete aruhusiwe  kuwahutubia jambo ambalo lilishindikana kwa wakati huo kutokana na sababu za kikanuni, ambapo kabla ya kuruhusiwa kuhutubiwa ilitakiwa kanuni zitenguliwe kwanza.

Spika Ndugai alijaribu kuwatuliza wabunge lakini ilishindikana waliendelea kushangilia huku wakiimba wimbo mpya wa Nay wa Mitego wa 'Wapo'.

Spika Ndugai alichagiza kwa kusema, katika historia ya Bunge haijawahi tokea mgeni akashangiliwa kama ilivyotokea kwa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete na kwamba hii imevunja rekodi.

Baada ya muda Spika aliwasihi wabunge kunyamaza ili shughuli za bunge ziendelee.

Kikwete akiwa na wasaidizi wake pamoja na mwanawe Ali waliondoka kupisha shughuli za Bunge ziendelee kwani angeendelea kuwemo bungeni utulivu ungeendelea kutoweka.HABARI NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

No comments:

Post a Comment