Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema akiwa kwenye gari baada ya kuachiwa kwa dhamana leo.
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) Godbless Lema, ameachiwa kwa dhamana leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.
Lema ameachiwa kwa dhamana ikiwa ni takribani miezi minne tangu awekwe rumande kwa kesi ya uchochezi.
Polisi wa kutuliza ghasia walijaa mahakamani hapo wakiwafukuza wafuasi wa Lema waliojaa katika viwanja vya mahakama hiyo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe walikuwepo mahakamani hapo leo.
No comments:
Post a Comment