Showing posts with label Naibu Waziri. Show all posts
Showing posts with label Naibu Waziri. Show all posts

Wednesday, November 30, 2016

NAIBU WAZIRI DR. KOLIMBA ATEMBELEA UBALOZI NAIROBI

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba, ambaye yuko Nairobi kuhudhuria kikao cha Bunge la Afrika Mashariki, ametumia fursa hiyo kutembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya na kuzungumza na watumishi.Katika kikao na Mhe. Waziri, watumishi wa Ubalozi walielezea changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika utendaji wa kazi, ikiwa ni pamoja na ufinyu wa bajeti. 

Hata hivyo watumishi hao walisema wameweza kukusanya maduhuli ya kuridhisha na kuhudumia Watanzania wanaopatwa na matatizo kwa kuchangishana wakati mwingine.Mhe. Kolimba alieleza kuridhishwa kwake na utendaji wa watumishi wa Ubalozi wa Nairobi na kuwapongeza kwa moyo wa kujitolea. 
Alisema Serikali itajitahidi kupatia balozi fedha na vifaa vya kazi kwa kadri ya uwezo wake, lakini akasisitiza watumishi wawe wabunifu na wajitolee kufidia pale upungufu unapojitokeza.Kikao cha Bunge la Afrika Mashariki kinachofanyika kwenye Bunge la Kenya kinatarajiwa kumalizika kesho.
Naibu Waziri, Dkt. Kolimba (kushoto) akifurahia bidhaa za Tanzania kwenye ofisi za Ubalozi wa Nairobi akiwa na Kaimu Balozi, Bi. Talha Mohamed Waziri.

Thursday, May 19, 2016

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI, DODOMA.

Waziri wa Nishati na Mdini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi mara walipokutana Bungeni mjini Dodoma wakati wa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madinileo 19 Me, 2016 bungeni hapo.