Showing posts with label Vietnam. Show all posts
Showing posts with label Vietnam. Show all posts

Thursday, March 10, 2016

RAIS WA VIETNAM MHE. TRUONG TANG SANG AMTEMBELEA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE.DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tang Sang akiwa pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi na wafanyakazi wa Ikulu mara baada ya kuwasili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tang Sang wakati walipokuwa wanazungumza Ikulu jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MKUU:TANZANIA YAINUKA KIUCHUMI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mabadiliko ya kiuchumi yaliyofanyika nchini yameifanya Tanzania ipige hatua kubwa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.
 "Kumekuwa na mabadiliko chanya kwenye ukuaji halisi wa Pato la Taifa, kushuka kwa mfumuko wa bei, na akiba ya kutosha ya fedha za kigeni. Pato la Taifa limekua kwa wastani wa asilimia 7 na mfumuko wa bei umeshuka hadi kufikia asilimia 5.3 mnamo Juni 2015 ikilinganishwa na asilimia 16 na asilimia 8 ilivyokuwa mwishoni mwa mwaka 2012 na mwanzoni wa mwaka 2013," alisema.