WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amesema mabadiliko ya kiuchumi yaliyofanyika nchini yameifanya
Tanzania ipige hatua kubwa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.
"Kumekuwa
na mabadiliko chanya kwenye ukuaji halisi wa Pato la Taifa, kushuka kwa mfumuko
wa bei, na akiba ya kutosha ya fedha za kigeni. Pato la Taifa limekua kwa
wastani wa asilimia 7 na mfumuko wa bei umeshuka hadi kufikia asilimia 5.3
mnamo Juni 2015 ikilinganishwa na asilimia 16 na asilimia 8 ilivyokuwa mwishoni
mwa mwaka 2012 na mwanzoni wa mwaka 2013," alisema.
