Thursday, January 05, 2017

MAKAMBA ATEUA WAJUMBE BODI YA NETFUND.

Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (anayeshughulikia Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba ameteua wajumbe wa Bodi ya wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Dhamana ya Hifadhi ya Mazingira Nchini (National Environmental Trust Fund - NETFUND).

Waziri huyo amefanya uteuzi huo jijini Dar es salaam kufuatia uamuzi wa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumteua Ali Mafuruki kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko huo.

WANUFAIKA 45,00 WAJITOKEZA KUREJESHA MIKOPO YAO BODI YA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU HESLB

Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imesema imeanza kupokea malipo kutoka kwa wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu wa miaka ya nyuma.
Wadaiwa hao wameibuka ikiwa ni siku saba tu, tangu bodi hiyo itangaze kiama kwa wadaiwa wote sugu wa walionufaika na mikopo ya bodi hiyo, ikiwa ni pamoja na kuanza kuchapisha majina na picha za wadaiwa hao kwenye vyombo vya habari, sambamba na kuunda tume ya kuwasaka wadai hao.

KATIBU MKUU WA CCM ABDURAHAMAN KINANA AZINDUA KAMPENI ZA CCM, DIMANI ZANZIBAR,

  Katibu Mkuu wa CCM,Andulrahman Kinana akimnadi Mgombea wa Ubunge jimbo la Dimani Juma Ali Juma, katika uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo hilo, mjini Zanzibar, Januari 5, 2017.

Wednesday, January 04, 2017

KAIMU KATIBU MKUU UVCCM SHAKA AZUNGUMZA NA WATUMISHI UVCCM MAKAO MAKUU

sak1
Kaimu Katibu Mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka  akizungumza na watumishi wa UVCCM  Makao Makuu   kutathmini utendaji wa jumuiya kwa mwaka 2016 na kupanga mikakati ya mwaka 2017 pamoja na kusikiliza michango  mawazo na changamoto mbali mbali zinazowakabili watumishi hao na namna ya kuzitatua ili mwaka 2017 uwe wa mafanikio zaidi.
sak2
”Tuongeze bidii ya kazi kila mmoja katika nafasi yake nilazima afahamu na kutambua ya kwamba kila mfanyakazi wa jumuiya katika eneo lake, mchango wake na juhudi za zake zinahitajika sana hasa katika hichi kipindi cha kuleta mageuzi makubwa ya kiutendaji kwa wanachama wetu ”Alisema  Kaimu Katibu Mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka wa kwanza kushoto akizungumza na watumishi wa UVCC Makao Makuu  Upanga Dar es Salaam leo.
sak3
:Mkuu wa Utawala UVCCM Ndg:Omary Ng’wanang’walu liposimama kuzungumza katika kikao hicho cha   kutathmini utendaji wa jumuiya kwa mwaka 2016 na kupanga mikakati ya mwaka 2017 leo Makao Makuu  UVCCM Upanga Dar es Salaam .
sak4
Kaimu Mkuu wa Idara ya Hamasa,Sera,Utafiti na Mawasiliano Ndg:Mtemi Sylvester Yaredi akizungumzia juu ya Mikakati ya Maswala Mbalimbali katika idara yake katika kikao hicho cha   kutathmini utendaji wa jumuiya kwa mwaka 2016 na kupanga mikakati ya mwaka 2017 leo Makao Makuu  UVCCM Upanga Dar es Salaam .
sak5
Kaimu Mkuu wa Idara ya Uchumi na Fedha Bi:Tumain Mwakasege akizungumzia juu ya Mikakati  Mbalimbali katika idara yake katika kikao hicho cha kutathmini utendaji wa jumuiya kwa mwaka 2016 na kupanga mikakati ya mwaka 2017 leo Makao Makuu  UVCCM Upanga Dar es Salaam
sak6
Mtumishi Wa Makao Makuu UVCCM Ndg:Pamphil James Hwago wa kwanza kushoto  akimuelezea Kaimu Katibu Mkuu Shaka wa kwanza kuli juu ya changamoto  za maswala mbali mbali yanayowakabili Watumishi Makao Makuu  UVCCM Upanga Dar es Salaam

Tuesday, January 03, 2017

MKUU WA MKOA WA ARUSHHA AKABIDHI MILIONI 624 VIKUNDI VYA WANAWAKE NA VIJANA MKOANI ARUSHA.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (katikati) akizungumza na vikundi vya wanawake na vijana kutoka katika Jiji la Arusha kabla ya Kukabidhi hundi za Mikopo ya robo ya kwanza na ya Pili kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.

WASIMAMIZI WA UCHAGUZI MDOGO ZINGATIENI SHERIA, KANUNI NA MAADILI, MSIKUBALI KUYUMBISHWA NA MTU.

 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw.kailima Ramadhani akifungua mafunzo ya siku 3 ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya jimbo na Kata na Maafisa wa Uchaguzi  mjini Dodoma. 

RAIS DKT MAGUFULI AWATAKA WAKUU WA WILAYA NA MIKOA KUONDOA UTITIRI WA KODI KATIKA MAZAO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Wakuu wa Mikoa,Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuondoa utitiri wa kodi uliopo kwenye Mazao ili wakulima waweze kunufaika kutokana na kujiongezea kipato.

Agizo hilo alimetolewa leo wakati akihutubia wakazi wa Wilaya ya Bukoba na watanzania kwa ujumla akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Kagera.

“Nawaagiza Wakuu wa Mikoa,Wilaya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri kupitia upya Kodi zilizopo katika bidhaa mbalimbali kama Kahawa na Pamba, hakikisheni mnaondoa utitiri huu wa Kodi ili wafanyabiashara hawa wafaidike na mazao yao,” Alisema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amewaahidi watanzania kuwa atahakikisha anafanya kazi usiku na mchana bila kujali itikadi, dini na makabila ili kuhakikisha nchi inasonga mbele katika nyanja zote za kimaendeleo.

Akizungumzia maendeleo ya michango mbalimbali kwa ajili ya wathirika wa tetemeko la Ardhi mkoani Kagera Rais Magufuli amesema kuwa mpaka sasa simenti iliyochangwa ni zaidi ya tani 30,600 na mabati zaidi ya elfu 31,000 ambapo wananchi wameshaanza kupewa na kujengea.

Amewahimiza wananchi walioathirika na tetemeko la Ardhi kutotegemea Serikali kuwafanyia kila kitu na badala yake waanze kujenga na watumie msimu huu wa mvua kulima ili kujipatia chakula.

Pia Rais Magufuli amewashukuru na kuwapongeza wahisani waliochangia Maafa ya Kagera na kuwataka kuendelea na moyo huo katika kulijenga Taifa letu.