Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (anayeshughulikia Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba ameteua wajumbe wa Bodi ya wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Dhamana ya Hifadhi ya Mazingira Nchini (National Environmental Trust Fund - NETFUND).
Waziri huyo amefanya uteuzi huo jijini Dar es salaam kufuatia uamuzi wa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumteua Ali Mafuruki kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko huo.
