Friday, June 24, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI ALIPOKABIDHIWA TAARIFA YA UCHAGUZI MKUU WA 2015 IKULU JIJINI DAR.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Damiani Lubuva wakiwa wameinua juu vitabu vya Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2015 wakati mwenyekiti huyo alipomkabidhi Rais taarifa hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam 

RISASI ZARINDIMA ZANZIBAR NA WATU WATATU WAJERUHIWA


Watu watatu wamejeruhiwa kwa kupigwa risasi na askari wa vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na kupelekwa hospitali ya Alrahma kwa matibabu.

Majeruhi hao ni Yussuf Ali Juma (23), Ali Shaame Ibrahim (18) na Salim Masoud Bakar (18), wakazi wa Tomondo Wilaya ya Magharibi Unguja.

Kabla ya watu hao kujeruhiwa, milio ya risasi ilitawala  majira ya saa 8:30 mchana katika mitaa ya Tomondo, Mwanakwerekwe na Kilimani, hivyo kuzua taharuki miongoni wakazi wa mitaa hiyo. 

Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa waliyaona magari ya vikosi hivyo yakiendeshwa kwa mwendo kasi kuzunguka maeneo hayo huku yakiwa na askari wakifyatua risasi.

“Mimi kwa sasa nipo hapa Kilimani na hivi punde tu risasi tumezisikia kutokea upande huu wa Mwanakwerekwe na Jang’ombe na ghafla naona watu wanakimbizwa kuletwa hapa Alrahma” alisema Rashid Said (54), mkazi wa Migombani ambaye ni dereva teksi.

Majeruhi Ibrahim alisema: “Walikuja wale mazombi, wengine walifunika uso waliwafungua ng’ombe wetu na kutaka kuwachukua, kwanza wakapiga risasi juu, tulipoona wanawapakiza katika magari lao tukasogea ndipo wakatupiga risasi.”

Bakari Juma (35), mkazi wa Msheleshelini alisema: “Tunasikia hawa jamaa wanataka wauze kitoweo cha nyama siku za sikukuu peke yao, lakini miye nasema sawa wafanye hivyo, ila si kwa ng’ombe wa kupora.”

Baadhi ya wananchi walidai kuwa mifugo hiyo wakiwamo ng’ombe wa maziwa ni mali yao.

Mmoja wa wafugaji hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Omar alisema: “Sisi tunafuga ng’ombe hawa kama mnavyoyaona mabanda yetu yapo si miaka kumi wala ishirini ni tangu zamani wakati huo Tomondo ni pori tupu na mpaka sasa mifugo yetu haizururi wala haimkeri mtu yeyote.”

Licha ya askari kudaiwa kufika eneo la tukio na katika hospitali walikolazwa majeruhi hao, hali ya usalama ilionekana kuyumba pale makundi ya watu yalipohamasika kusogelea maeneo hayo.

Waliofika katika hospitali hiyo ni pamoja na Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano kwa Umma wa Chama cha Wananchi (CUF), Salim Abdalla Bimani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kufuatilia zaidi ili kubaini chanzo chake.

Hata hivyo, alisema polisi waliingilia kati na kwenda katika maeneo hayo kurejesha hali ya usalama.

“Sijapata kwa ukamilifu kilichotokea, lakini ni kweli hawa vikosi wanaendesha operesheni ya kukamata ng’ombe wanaozurura mitaani, wamekwenda huko na kukatokea kukwaruzana baada ya kuwepo vijana ambao hawataki kuondoa ng’ombe, nimepeleka askari kutuliza hali na sasa hali imekuwa ya amani”, alisema Kamanda Mkadam.

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YAKABIDHIWA MAGARI TISA.

 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa pamoja na mwakilishi wa katibu Mkuu wa Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Claud Kumalija wakionyesha ufunguo wa gari mbele ya waandishi wa habari na wageni waalikwa kuashiria kupokea magari tisa yaliyotolewa na Shirika la ICAP Tanzania kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utakaofanyika nchi nzima kuanzia mwezi Septemba, 2016.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA BALOZI WA NORWAY, FINLAND NA MJUMBE MAALUM KUTOKA OFISI YA WAZIRI MKUU WA MALAYSIA, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na balozi wa Norway hapa nchini Hanne-Marie Kaarstand watatu kutoka kushoto mara baada ya kumaliza mazungumzo  yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Norway hapa nchini Hanne-Marie Kaarstand Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Norway hapa nchini Hanne-Marie Kaarstand mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisoma barua ya pongezi iliyowasilishwa kwake na Waziri kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia Dato Sri Idris Jala ambaye ni Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Malaysia.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Waziri kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia Dato Sri Idris Jala ambaye ni Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Malaysia mara baada ya kumkabidhi barua hiyo ya pongezi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia Dato Sri Idris Jala ambaye ni Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Malaysia mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU AKUTANA NA WAZIRI KUTOKA MALAYSIA NA MAKAMU WA RAIS WA TIGO AFRIKA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na Waziri asiye na Wizara Maalum katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia na Mkurugenzi Mtendaji wa kitengo kinachoshughulikia masuala ya utendaji Na utekelezaji wa miradi ya serikali Dk. Sri Idris Jala ,Ikulu jijini Dar es Salaam.

Thursday, June 23, 2016

RAIS KAGAME KUFUNGUA MAONESHO YA 40 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM-2016


Ofisa Mawasiliano Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Theresa Chilambo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam  asubuhi wakati akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka (katikati), kuzungumza na wanahabari kuhusu maonesho ya 40 ya biashara ya kimataifa yatakayoanza rasmi Juni 28, 2016 hadi Julai 8, 2016 katika viwanja vya Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Ukuzaji wa Biashara, Anna Bulondo.

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI AZUNGUMZIA MATUKIO YA KIHALIFU YALIYOTOKEA MKOA WA KUSINI PEMBA


Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusiana na matukio ya kihalifu ya kuchoma moto nyumba, mashamba na kuharibu mazao yaliyotokea mkoa wa Kusini Pemba na kuahidi kuyashughulikia. Kulia ni Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omary Makame.