Showing posts with label Gas and Metals National Corporation (JOGMEC). Show all posts
Showing posts with label Gas and Metals National Corporation (JOGMEC). Show all posts

Thursday, August 04, 2016

WAZIRI MHONGO ATEMBELEWA NA BALOZI WA JAPAN NCHINI TANZANIA.

BALOZI wa Japan nchini Tanzania, Masaharn Yoshida amemtembelea Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi zao hususan katika sekta ya nishati.

Balozi Yoshida, aliyeambatana na Ujumbe wa baadhi ya maofisa kutoka Ubalozini na wataalam kadhaa kutoka Shirika la Japan Oil, Gas and Metals National Corporation (JOGMEC), alimtembelea Prof Muhongo Agosti 3 mwaka huu ofisini kwake, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa tatu kutoka kulia) akizungumza na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharn Yoshida (Kulia kwa Waziri) na Ujumbe wake, walipomtembelea Waziri ofisini kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni.