Showing posts with label wizara ya Nishati na Madini. Show all posts
Showing posts with label wizara ya Nishati na Madini. Show all posts

Tuesday, May 10, 2016

USAMBAZAJI WA NISHATI YA UMEME UNAOFANYWA NA WAKALA WA NISHATI VIJIJINI (REA) UMEWEZESHA WANANCHI WENGI VIJIJINI

Na Jovina Bujulu-MAELEZO

USAMBAZAJI wa nishati ya umeme unaofanywa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umewezesha Wananchi wengi walioko vijijini kuanzisha miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa REA nchini Dkt. Lutengano Mwakahesya, nishati bora inachangia ukuaji wa uchumi wa Taifa jambo ambalo linasaidia kuboresha hali ya maisha ya Wananchi wengi walio vijijini. Kwa kutambua umuhimu huo REA kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali imeweza kuibua miradi mbalimbali ya nishati vijijini ili Wananchi waweze kufaidika nayo.

Wadau hao ni pamoja na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa Bei za Bidhaa (EWURA), Wizara ya Nishati na Madini, Asasi zisizo za Kiserikali (AZISE), Asasi za Kijamii (AZAKI) na Sekta binafsi. Dkt. Mwakahesya ameainisha miradi ya nishati za umeme kuwa ni pamoja na zile zinazotumia nguvu ya upepo, jua, maji na bayogasi.

Dkt. Lutengano ameeleza kwamba, lengo kubwa la ushirikiano baina ya REA na Wadau hao ni kuibua miradi mbalimbali ya nishati,  kutoa ruzuku na kuwezesha upatikanaji wa ushauri wa kitaaluma kwa waendelezaji wenye sifa katika masuala ya kiufundi, usimamiaji, uchanganuzi wa kifedha,  ugharamiaji wa miradi na mienendo mizuri ya miradi hiyo. 

Friday, April 08, 2016

PROFESA MUHONGO ASISITIZA MAPINDUZI YA KIUCHUMI KATIKA SEKTA YA NISHATI NA MADINI.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhungo akizungumza na wafanyakazi wa wizara ya nishati na madini na kufungua baraza la wafanyakazi wa wizara yake katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la wafanyazaki wa wizara ya Nishati na Madini, Selina Msumbushi akizungumza na wafanyakazi wa wizara ya nishati na madini na kusoma mapendekezo ya wafanyakazi hao leo katika mkutano wa kufungua baraza la wafanyakazi uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.