Thursday, June 16, 2016

MANISPAA YA ILALA YAENDELEA KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA WA WATOTO:


Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala Bi. Tabu Shaibu akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Ulinzi na Usalama wa Mtoto kuelekea Siku ya Mtoto wa Afrika inayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka. Kushoto ni Afisa Ustawi wa Amana One Stop Centre Bw. Sophian Mndolwa na kulia ni Mratibu wa Timu ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto Manispaa ya Ilala Bw. Waziri Nashiri.

Tuesday, June 14, 2016

JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM KUPINGA KONGAMANO LA ACT WAZALENDO

DAR ES SALAAM
Jeshi la polisi kanda maalum ya dar  es salaam limepinga kongamano lililo pangwa kufanyika katika ofisi za chama cha act wazalendo  yaliyo andaliwa na kiongozi wa chama hicho Mh Zito Zuberi Kabwe kwa kusema maandamano hayo uweza kuchochea uvunjifu wa amani.

VICTORIA MUNGURE

TUNDU LISSU NA MHARIRI WA MAWIO KIZIMBANI LEO KWA UCHOCHEZI:


Serikali itawafikisha Mahakama ya Kisutu, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na mmiliki wa gazeti lililofungiwa la Mawio, Simon Mkina kwa kuandika habari za uchochezi.

Mkina alisema baada ya kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi kuwa kwa mara ya kwanza watafikishwa mahakamani.

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AAPISHWA NA KUPOKELEWA MAKAO MAKUU YA WIZARA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh, Mwigulu Nchemba(kulia), na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni, muda mfupi baada ya Rais Dkt. John Magufuli kumwapisha Waziri Mwigulu Nchemba kuongoza wizara hiyo.

MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI, JOSHUA NASSARI NA MADIWANI WANNE WAFIKISHWA MAHAKAMANI


MBUNGE wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari na wenzake wanne ambao ni madiwani wa Halmashauri ya Meru wilayani Arumeru, wamesomewa shitaka la kuharibu uzio eneo la Leganga wilayani humo. 

Walisomewa shitaka lao mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Augustine Rwezile jana.

MAAFISA WAKUU NCHINI UGANDA WAMEKABILIANA NA KUNDI WALIOKUWA WAMEJIHAMI KWA SILAHA:

UGANDA Maafisa wakuu nchini Uganda wanasema kuwa walinda usalama wamekabiliana vikali na kundi moja la watu, waliokuwa wamejihami kwa silaha, waliojaribu kuvamia kituo cha polisi kilichoko katikati mwa Gulu. Polisi inaamini kuwa shambulio hilo lilikuwa njama za kujaribu kumuokoa mwanasiasa mmoja wa upinzani anayezuliwa- Dan Oola Odiya.Wanasema kuwa milio ya risasi ilidumu kwa muda wa dakika thelathini. Taharuki ya kisiasa imetanda nchini Uganda, kufuatia matokeo tata ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Februari mwaka huu. nimezungumza na mchambuzi wa masuala ya kisisa Abdulkarim Atiki.... .insert Juma lililopita, jeshi la Uganda liliwatia mbaroni askari thelathini na raia kadhaa, likisema kuwa walikuwa na njama ya kuunda kundi la waasi.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AGAWA FUTARI KWA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM NA KUJIONEA MABASI YA MWENDO KASI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteremka kwenye basi la mwendo kasi baada ya kupanda na kujionea ubora na uzuri wa mabasi hayo ambayo yamerahisisha usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.( Picna na OMR)