Showing posts with label Uganda. Show all posts
Showing posts with label Uganda. Show all posts
Tuesday, June 14, 2016
MAAFISA WAKUU NCHINI UGANDA WAMEKABILIANA NA KUNDI WALIOKUWA WAMEJIHAMI KWA SILAHA:
UGANDA
Maafisa wakuu nchini Uganda wanasema kuwa walinda usalama wamekabiliana vikali na kundi moja la watu, waliokuwa wamejihami kwa silaha, waliojaribu kuvamia kituo cha polisi kilichoko katikati mwa Gulu.
Polisi inaamini kuwa shambulio hilo lilikuwa njama za kujaribu kumuokoa mwanasiasa mmoja wa upinzani anayezuliwa- Dan Oola Odiya.Wanasema kuwa milio ya risasi ilidumu kwa muda wa dakika thelathini.
Taharuki ya kisiasa imetanda nchini Uganda, kufuatia matokeo tata ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Februari mwaka huu.
nimezungumza na mchambuzi wa masuala ya kisisa Abdulkarim Atiki....
.insert
Juma lililopita, jeshi la Uganda liliwatia mbaroni askari thelathini na raia kadhaa, likisema kuwa walikuwa na njama ya kuunda kundi la waasi.
Tuesday, May 10, 2016
MEGAWATI 100 KUTOKANA NA JOTOARDHI KUZALISHWA MIAKA 7 IJAYO:
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati, Dk. Juliana Pallangyo (pichani) akisoma hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa siku tatu jijini Dar es Salaam uliokutanisha wataalam kutoka nchi mbalimbali kwa ajili ya kujadili taarifa ya mtaalam mwelekezi kuhusu utafiti uliofanywa katika Ziwa Ngozi lililopo mkoani Mbeya ambapo kuna viashiria vya jotoardhi pamoja na eneo la Kibiro nchini Uganda.
Subscribe to:
Posts (Atom)