Mbunge wa Dodoma Mjini na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde amefanya ziara ya kushtukiza katika kambi tiba ya GSM Foundation inayofanywa na kikosi cha Madaktari bingwa kutoka hospitali ya MOI, ambayo kuanzia imepiga kambi Dodoma baada ya kutoka katika mikoa ya Mwanza, Singida, na Shinyanga.
