Thursday, December 01, 2016
KAMISHNA WA TRA AHITIMISHA MAFUNZO YA ‘SCANNER’ MPYA BANDARINI
Kamishna wa Mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya usimamizi na uendeshaji wa mashine za ukaguzi wa mizigo ‘scanner’ kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na TRA. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA, Bw. Abdulrahman Mbamba pamoja na Wakufunzi kutoka Kampuni iliyofunga mashine hizo.Wednesday, November 30, 2016
UNESCO-TANZANIA YAWAJENGEA UWEZO MAAFISA KUTOKAWIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO KATIKA KUTEKELEZA MPANGO MKAKATI WA WIZARA MAWAKA 2016/2017

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, (UNESCO), nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigueas, (kulia), akiendesah semina ya mafunzo ya siku tatu kujenga uwezo kwa maafisa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, makao makuu ya UNESCO, Oysterbay jijini Dares Salaam, leo Novemba 30, 2016. Kushoto ni Mwanasheria wa Wizara, Bw.Evordy Kyando.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni , (UNESCO), limeendesha mafunzo ya siku tatu kwa maafisa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ili kuwajengea uwezo wa kutekeelza mpango mkakati wa wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017.Mafunzo hayo yaliyoanza leo Novemba 30, 2016, na kuendeshwa na Mkuu wa Ofisi ya UNESCO, nchini, Bi. Zulmira Rodrigues yanafanyika kwenye ofisi za shirikahilo,Oysterbay jijini Dar es Salaam.
NAIBU WAZIRI DR. KOLIMBA ATEMBELEA UBALOZI NAIROBI
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba, ambaye yuko Nairobi kuhudhuria kikao cha Bunge la Afrika Mashariki, ametumia fursa hiyo kutembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya na kuzungumza na watumishi.Katika kikao na Mhe. Waziri, watumishi wa Ubalozi walielezea changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika utendaji wa kazi, ikiwa ni pamoja na ufinyu wa bajeti.
Hata hivyo watumishi hao walisema wameweza kukusanya maduhuli ya kuridhisha na kuhudumia Watanzania wanaopatwa na matatizo kwa kuchangishana wakati mwingine.Mhe. Kolimba alieleza kuridhishwa kwake na utendaji wa watumishi wa Ubalozi wa Nairobi na kuwapongeza kwa moyo wa kujitolea.
Alisema Serikali itajitahidi kupatia balozi fedha na vifaa vya kazi kwa kadri ya uwezo wake, lakini akasisitiza watumishi wawe wabunifu na wajitolee kufidia pale upungufu unapojitokeza.Kikao cha Bunge la Afrika Mashariki kinachofanyika kwenye Bunge la Kenya kinatarajiwa kumalizika kesho.
Naibu Waziri, Dkt. Kolimba (kushoto) akifurahia bidhaa za Tanzania kwenye ofisi za Ubalozi wa Nairobi akiwa na Kaimu Balozi, Bi. Talha Mohamed Waziri.
Tuesday, November 29, 2016
SERIKALI YAMPOKONYA SUMAYE SHAMBA LAKE LENYE UKUBWA WA HEKTA 33
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amepokonywa na Serikali shamba lake lenye ukubwa wa hekta 33 kwa kile kilichoelezwa kushindwa kuliendeleza.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amesema kuwa Serikali imefikia uamuzi huo baada ya Sumaye kushindwa kuliendeleza kama notisi ya siku 90 ilivyoeleza.
RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA ZAMBIA EDGAR CHAGWA LUNGU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
Friday, November 25, 2016
SIMBACHAWENE AAGIZA FEDHA ZA TASAF ZILIZOTOLEWA KWA KAYA ZISIZOKUWA NA SIFA KUREJESHWA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene ameziagiza Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya kuhakikisha kuwa fedha zilizotolewa kwa kaya zisizokuwa na sifa katika Mpango wa kunusuru kaya maskini unaofanywa kwa uratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF) kurejeshwa ili ziweze kuwanufaisha walengwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)



