Monday, April 04, 2016

KAMPUNI YA SIRI YAWAHUSISHA VIONGOZI 72 DUNIANI:


Image captionNyaraka za siri zilizopatikana zaonesha kuwa viongozi 72 kote duniani wanatumia kampuni moja kutakatisha fedha kukwepa kodi

Stakabadhi za siri za shirika moja la kisheria la Panama zilizopatikana na gazeti moja la Ujerumani zimeonyesha viongozi zaidi ya 72 wakuu wa nchi wa zamani na wale waliopo madarakani wanahusika na kampuni hiyo ya kisiri iliyowasaidia wateja wao kukwepa kulipa kodi, utakatishaji fedha, kukiuka mikataba na vikwazo vya kiuchumi vya kimataifa.

WAHAMIAJI WAANZA KUFURUSHWA UGIRIKI:

Uturuki

Image copyrightAP
Image captionUturuki inatarajia kupokea wahamiaji 500

Maboti ya kwanza yaliyowabeba wahamiaji ambao wanafurushwa kutoka Ugiriki na kupelekwa Uturuki yameanza safari chini ya mpango wa EU unaotarajiwa kupunguza idadi ya wahamiaji wanaoingia Ulaya.
Mamia ya wahamiaji wameonekana wakiabiri feri katika kisiwa cha Lesbos nchini Ugiriki mapema Jumatatu.
Wanapelekwa Dikili, magharibi mwa Uturuki.

TBS WAVAMIA BEKARI YA MBUNGE WA CCM SULEIMAN SADDIQ MURAD NA KUIFUNGIA KWA MUDA USIOJULIKANA:


Mzimu umeendelea kumwandama Mbunge wa Mvomero, Suleiman Saddiq Murad. 

Baada  ya  TAKUKURU  kumpandisha  mahakamani wiki iliyopita  kwa kuomba rushwa ya milioni 30, shirika la Viwango Tanzania (TBS)  nalo limeifunga Bekari yake( tanuri mikate )   kwa muda usiojulikana kwa kutotimiza masharti  ya viwango vya ubora.

KAYA 40 ZAKOSA MAKAZI BAADA YA NYUMBA ZAO KUBOMOLEWA NA MAFURIKO YA MVUA:

Mvua  kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia juzi imeleta athari kubwa katika Kijiji cha Chenene Kata ya Haneti Tarafa ya Itiso, Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma na kukosesha makazi zaidi ya kaya 40.

Akizungumza jana, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Farida Mgomi alisema nyumba nyingi zilizobomoka ni zile zilizojengwa kwa matofali ya udongo. Mgomi alisema athari hiyo inaweza kuongezeka kutokana na nyumba kujaa maji na zinaposhindwa kuhimili hudondoka.

HALIMA MDEE AMTAKA RAIS MAGUFULI ATAJE POSHO NA MARUPURUPU ANAYOPOKEA BAADA YA KUTAJA MSHAHARA WAKE:


Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee amemuomba Rais John Magufuli kuweka wazi posho na marupurupu anayoyapata ili Watanzania wajue kiasi halisi anachokipata mbali na mshahara wake.

MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA AMKAMUA JIPU MHANDISI WA MANISPAA,AMSWEKA RUMANDE HUKU MKURUGENZI WAKE AKISHUHUDIA:

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amemsweka rumande Muhandisi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Simoni Ngagani, baada ya kupuuza agizo lake la kufanya maandalizi mapema ya kununua kokoto na Saruji kwa ajili ya kusimika mapipa 50 ya kutunzia uchafu kwenye mitaa mbalimbali katika manispaa ya Shinyanga ikiwemo eneo kituo cha mabasi yaendayo wilayani.
Choo cha stendi ya mabasi yaendayo wilayani kikiwa kimezungukwa na uchafu yakiwemo maji machafu yaliyotuama,pichani ni afisa mazingira wa manispaa ya Shinyanga Elly Nakuzelwa akiingia katika choo hicho.

WAZIRI KITWANGA AGAWA BAISKELI 120 KWA MAKATIBU WA MATAWI CCM JIMBONI KWAKE MISUNGWI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kulia) akimkabidhi Baiskeli 120 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 22, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu kwa ajili ya kuwakabidhi makatibu wa matawi wa CCM Jimbo la Misungwi ili ziweze kutumika kwa ajili ya shughuli za chama jimboni humo. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ofisi ya Wilaya ya Chama hicho, mjini Misungwi.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu (kushoto)