Showing posts with label Charles Kitwanga. Show all posts
Showing posts with label Charles Kitwanga. Show all posts

Wednesday, June 22, 2016

KITWANGA AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA......ASEMA YALIYOTOKEA ANAMWACHIA MUNGU, WIKI IJAYO KUTUA BUNGENI KWA KISHINDO


ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, amesema yupo imara na amerejea nchini akiwa na matumaini mapya.

Pamoja na hali hiyo, amesema kuwa hivi sasa anajipanga kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha anaisaidia nchi pamoja na wapigakura wake na kuwa na maendeleo ya kweli na Jumatano ya Julai 29, ataripoti bungeni.

Thursday, April 07, 2016

KITWANGA ATAKA MADAKTARI, WAUGUZI WANAOJIHUSISHA NA RUSHWA WACHUKULIWE HATUA KALI JIMBONI KWAKE.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (aliyevaa koti) akicheza ngoma ya asili na wananchi wa Kata ya Sumbugu wilayani Misungwi mara baada ya kuwasili katika eneo hilo kwa ajili ya kufungua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi hao. Waziri Kitwanga amemaliza ziara jimboni kwake leo na kuwaonya madaktari na wauguzi wilayani humo kuacha tabia ya kuwaomba rushwa wananchi. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akizungumza na wananchi wa Kata ya Sumbugu wilayani Misungwi. Katika hotuba yake, Kitwanga aliwataka wananchi wa jimbo lake washirikiane ili kuliletea maendeleo jimbo hilo na kuwaonya madaktari na wauguzi wilayani humo kuacha tabia ya kuwaomba rushwa wananchi. Kitwanga amemaliza ziara jimboni kwake.  

Monday, April 04, 2016

WAZIRI KITWANGA AGAWA BAISKELI 120 KWA MAKATIBU WA MATAWI CCM JIMBONI KWAKE MISUNGWI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kulia) akimkabidhi Baiskeli 120 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 22, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu kwa ajili ya kuwakabidhi makatibu wa matawi wa CCM Jimbo la Misungwi ili ziweze kutumika kwa ajili ya shughuli za chama jimboni humo. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ofisi ya Wilaya ya Chama hicho, mjini Misungwi.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu (kushoto)