Showing posts with label Dk Wilhem Ngasamiaku. Show all posts
Showing posts with label Dk Wilhem Ngasamiaku. Show all posts

Sunday, April 24, 2016

SERIKALI YAWAKALIA KOONI WATUMISHI WAZEMBE NA WABADHILIFU:


Serikali imesema kuanzia sasa mtumishi wa umma atakayeshindwa kusimamia rasilimali za umma, achague moja kati ya mawili, kuacha kazi au atumbuliwe.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango wakati alipozindua kitabu cha mwongozo wa usimamizi wa rasilimali za umma unaolenga kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa na kusimamiwa vizuri kwa maslahi ya Taifa.