Showing posts with label Mwenyekiti wa ACT. Show all posts
Showing posts with label Mwenyekiti wa ACT. Show all posts

Tuesday, April 26, 2016

RAIS MAGUFULI BADO HAJAGUSA KANSA YA UFISADI


Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amemtaka Rais John Magufuli kukabiliana na vikundi vya mafisadi vinavyoiba mabilioni ya fedha za umma kupitia mikataba mibovu waliyoingia badala ya kuishia kutumbua majipu. 
 
Akizungumza katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama chake jana, Zitto alisema ACT Wazalendo inaunga mkono jitihada za Rais Magufuli katika kupambana na ufisadi, lakini bado hajagusa kiini chenyewe.