Showing posts with label Kifua Kikuu (TB). Show all posts
Showing posts with label Kifua Kikuu (TB). Show all posts

Thursday, March 24, 2016

USHAURI WATOLEWA KWA VITUO BINAFSI VYA HUDUMA ZA AFYA KUTOA HUDUMA TIBA YA KIFUA KIKUU:


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Mhe. Ummy Mwalimu ametoa Rai kwa wamiliki wa vituo binafsi vya kutoa huduma za afya kupanua wigo wa huduma na kutoa matibabu ya Kifua Kikuu katika taasisi zao.

Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri huyo wakati akitoa tamko katika kuadhimisha siku ya Kifua Kikuu duniani ambapo ufanyika tarehe 24 Machi kila mwaka.

Monday, March 21, 2016

Mbunge Wa Kigamboni Dkt Ndugulile Achaguliwa Kuwa Mwenyekiti Wa Kamati Ya Ushauri Ya Masuala Ya Ukimwi, Afya Ya Kina Mama Na Watoto Ya Mabunge Duniani


MBUNGE wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya masuala ya Ukimwi, Afya ya Mama na Watoto ya Taasisi ya Mabunge Duniani (IPU). Dk Ndugulile amechaguliwa katika mkutano wa 134 wa Mabunge duniani unaoendelea mjini Lusaka, Zambia.

Mkutano huo ulioanza Machi 17, mwaka huu unatarajia kuisha keshokutwa. Kabla ya kuchaguliwa kwake, Dk Ndugulile alikuwa ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo. 

Kamati hiyo inajumuisha wabunge wasiozidi 12 ambao huteuliwa na Rais wa IPU kutokana na umahiri na mchango wao katika masuala ya Ukimwi na masuala ya afya ya mama na watoto.

Wajumbe wengine wa kamati hiyo wanatoka nchi za Armenia, India, Bangladesh, Afrika Kusini, Rwanda, Italia, Ubelgiji, Austria, Sweden, Dominica na Marekani. 

Majukumu ya Kamati hiyo ni kushauri, kujengea uwezo na kuhamasisha mabunge duniani kuhusiana na njia bora za kuboresha huduma za Ukimwi pamoja na afya za akinamama na watoto.

Dk Ndugulile ni daktari bingwa katika magonjwa ya maambukizi na pia kwenye afya ya jamii. Pamoja na majukumu hayo mapya, pia mbunge huyo ni Mwakilishi wa bara la Afrika katika Taasisi ya Kimataifa ya Ukimwi, Mjumbe wa Kamati ya Wabunge Duniani kuhusu masuala ya Kifua Kikuu (TB) na Mwakilishi wa Bunge la Tanzania kwenye Bunge la Afrika.