Showing posts with label watu sita wafariki dunia. Show all posts
Showing posts with label watu sita wafariki dunia. Show all posts

Monday, March 21, 2016

WATU SITA WAPOTEZA MAISHA NA WENGINE KUJERUHIWA VIBAYA KUFUATIA AJALI YA LORI KUYAGONGA MAGARI MATATU YA MSAFARA WA KAMATI YA TAMISEMI ENEO LA KEREGE, BAGAMOYO.


WATU sita  wanahisia kufariki dunia huku 12 wakiwa wamejeruhiwa vibaya, katika ajali iliyoyahusisha magari manne, mawili yakiwa katika msafara wa Kamati ya Bunge Utawala na TAMISEMI maeneo ya Kerege, Bagamoyo Pwani, anaandika Mwandishi Wetu.

Ajari hiyo iliyohusisha lori la mchanga, gari dogo yaliyokuwa yanatokea Bagamoyo kuja Dar es Salaam, na magari mawili yaliyokuwa kwenye msafara wa Kamati hiyo, yaliyokuwa yanaenda Bagamoyo kwa shughuli zake za kibunge.

Magari yaliyokuwa katika msafara wa kamati hiyo, ni gari la Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na gari la Mkurugenzi wa Wilaya ya Bagamoyo ambayo yaligongwa na lori hilo la mchanga na kusababisha vifo vya watu hao na kuwajeruhi wengine kadhaa.