
WATU sita wanahisia kufariki dunia huku 12 wakiwa wamejeruhiwa vibaya, katika ajali iliyoyahusisha magari manne, mawili yakiwa katika msafara wa Kamati ya Bunge Utawala na TAMISEMI maeneo ya Kerege, Bagamoyo Pwani, anaandika Mwandishi Wetu.
Ajari hiyo iliyohusisha lori la mchanga, gari dogo yaliyokuwa yanatokea Bagamoyo kuja Dar es Salaam, na magari mawili yaliyokuwa kwenye msafara wa Kamati hiyo, yaliyokuwa yanaenda Bagamoyo kwa shughuli zake za kibunge.
Magari yaliyokuwa katika msafara wa kamati hiyo, ni gari la Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na gari la Mkurugenzi wa Wilaya ya Bagamoyo ambayo yaligongwa na lori hilo la mchanga na kusababisha vifo vya watu hao na kuwajeruhi wengine kadhaa.