Showing posts with label shule ya Msingi Nyangao. Show all posts
Showing posts with label shule ya Msingi Nyangao. Show all posts

Monday, April 18, 2016

HALMASHAURI YATENGA BAJETI YA MILIONI 162 KUISAIDIA SHULE YA WALEMAVU

Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
Halmashauri ya Wilaya ya Lindi iliyopo Mkoa wa Lindi imetenga jumla ya shilingi milioni 162 katika mwaka wa fedha 2016/17 kwa ajili ya kuisaidia shule ya Msingi Nyangao.
Hayo yamesemwa  na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi. Olliver Vavunge alipokuwa akikanusha kuhusu madai ya wazazi kutaka shule hiyo ifungwe kwa sababu ya ukosefu wa huduma muhimu.
“Kwa kuwa shule hiyo tayari ina mabweni pamoja na bwalo la chakula, katika bajeti iliyotengwa na Halmashauri kwa mwaka huu wa fedha jumla ya shilingi milioni 100  zitatumika katika ujenzi wa uzio wa shule pamoja na marekebisho madogo madogo ya shule hiyo na shilingi milioni 62 zitatumika kwa ajili ya chakula”alisema Bi. Olliver