Showing posts with label fisa habari wa Manispaa ya Ilala Bw. David Langa. Show all posts
Showing posts with label fisa habari wa Manispaa ya Ilala Bw. David Langa. Show all posts

Thursday, May 05, 2016

WAKAZI WA ILALA WAHAKIKISHIWA USALAMA;

Jeshi la polisi Mkoa wa kipolisi Ilala limewahakikishia usalama wananchi wa Mkoa wa kipolisi Ilala  na kuachana na taarifa za uvumi kuhusu hali ya usalama katika mkoa huo wa kipolisi.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Lucas Mkondya  amesema kuwa Jeshi la Polisi limejipanga ipasavyo kukabiliana na uhalifu wa aina yoyote na kutoa tahadhari kwa wahalifu kuwa makini kwani jeshi lake limejidhatiti ipasavyo.