Jeshi la polisi Mkoa wa kipolisi Ilala limewahakikishia usalama wananchi wa Mkoa wa kipolisi Ilala na kuachana na taarifa za uvumi kuhusu hali ya usalama katika mkoa huo wa kipolisi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Lucas Mkondya amesema kuwa Jeshi la Polisi limejipanga ipasavyo kukabiliana na uhalifu wa aina yoyote na kutoa tahadhari kwa wahalifu kuwa makini kwani jeshi lake limejidhatiti ipasavyo.
