Showing posts with label Simon Sirro. Show all posts
Showing posts with label Simon Sirro. Show all posts

Tuesday, April 26, 2016

JESHI LA POLISI LAWATIA MBARONI OMBAOMBA 45 KATIKA JIJI LA DAR ES SALAA NA 17 WAPELEKWA GEREZANI


Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, wamewakamata na kuwaondoa ombaomba 45 na 17 wamewapeleka gerezani. 
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema jana kuwa jeshi hilo kwa kushirikiana na Idara ya Ustawi wa Jamii, wanafanya utaratibu wa kuhakikisha watu hao wanarudishwa mikoani walikotoka. 
 
“Kazi hii inaenda vizuri na ombaomba wachache wamebakia ambao wakiwaona askari wanakimbia na kutokomea kusikojulikana,”alisema Sirro.