Showing posts with label Rais mstaafu wa Awamu ya Nne. Show all posts
Showing posts with label Rais mstaafu wa Awamu ya Nne. Show all posts

Thursday, November 17, 2016

JK AWATUNUKU DIGRII WAHITIMU 1,179 CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU DUCE

 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (wa pili kulia) akimkabidhi zawadi mwanafunzi bora wa Chuo Kikuu Kishiriki cha  Elimu Dar es Salaam (Duce), Haji Mohamed wakati wa Mahafali ya Tisa ya chuo hicho leo. Jumla ya wanafunzi 1,179 walihitimu na kutunukiwa digrii za awali.

Sunday, April 24, 2016

MAALIM SEIF AENDELEA KULIA NA KIKWETE KWA KUPINDUA MATOKEO UCHAGUZI MKUU WA ZANZIBAR.


Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad ameendelea kumtupia lawama Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete akidai kuwa alitumia dola ‘kupindua’ demokrasia ili kuinusuru CCM iliyokuwa imebwagwa kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita.

Alisema Kikwete ambaye wakati huo alikuwa Amiri Jeshi Mkuu, anastahili lawama kwa madai kuwa alituma vyombo vya dola kugeuza uamuzi wa Wazanzibari waliokuwa wameufanya kupitia masanduku ya kura Oktoba 25 mwaka jana.

Tuesday, March 15, 2016

MABALOZI WA NCHI MBALI MBALI ZA AFRIKA WAKUTANA NA RAIS MSTAAFU JAKAYA MRISHO KIKWETE:

Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, akizungumza na Mabalozi mbalimbali wa Afrika wanaoziwakilisha nchi zao nchini, walipofika nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo kumpa mkono wa pole kutokana na kifo cha Kaka yake, Suleima Kikwete, kilichotokea hivi karibuni.
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (katikati), akifurahi jambo na Mabalozi mbalimbali wa Afrika wanaoziwakilisha nchi zao nchini, walipofika nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo kumpa mkono wa pole kutokana na kifo cha Kaka yake, Suleima Kikwete, kilichotokea hivi karibuni. (PICHA NA KASSIM MBAROUK).