Showing posts with label Mkuu wa Mkoa wa Kigoma. Show all posts
Showing posts with label Mkuu wa Mkoa wa Kigoma. Show all posts

Tuesday, July 05, 2016

MKUU WA MKOA WA KIGOMA BRIGEDIA JENERALI EMMANUEL MAGANGA AZINDUA MRADI WA UIMARISHAJI WA MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA (PS3)

 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali (Rt), Emmanuel Maganga akizindua mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) katika mkoa wake wa Kigoma leo. Mradi huo wa miaka mitano unafadhiliwa na Shirika la Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID)  na utatekelezwa katika mikoa 13 nchini na kushirikisha Halamashauri 93.

Friday, March 25, 2016

WATUMISHI HEWA 169 WAGUNDULIKA KIGOMA.....MKUU WA MKOA AWATAKA WAKURUGENZI KUBAINISHA KIASI WALICHOLIPWA MWAKA MZIMA.


Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Emanuel Maganga amewataka wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote waliopo katika halmashauri zote kutaja kiasi cha fedha kilichotumika kuwalipa mishahara watumishi hewa 169 kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Akiongea na waandishi wa habari, Brigedia Jenerali Emanuel Maganga alisema kuwa agizo hilo ni kufuatia agizo la Mheshimwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli la kufanya uhakiki wa watumishi katika halmashauri zote ili kuwabaini watumishi hewa wanaolipwa mishahara kinyume na utaratibu za utumishi.