Showing posts with label Brigedia Jenerali Emanuel Maganga. Show all posts
Showing posts with label Brigedia Jenerali Emanuel Maganga. Show all posts

Friday, March 25, 2016

WATUMISHI HEWA 169 WAGUNDULIKA KIGOMA.....MKUU WA MKOA AWATAKA WAKURUGENZI KUBAINISHA KIASI WALICHOLIPWA MWAKA MZIMA.


Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Emanuel Maganga amewataka wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote waliopo katika halmashauri zote kutaja kiasi cha fedha kilichotumika kuwalipa mishahara watumishi hewa 169 kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Akiongea na waandishi wa habari, Brigedia Jenerali Emanuel Maganga alisema kuwa agizo hilo ni kufuatia agizo la Mheshimwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli la kufanya uhakiki wa watumishi katika halmashauri zote ili kuwabaini watumishi hewa wanaolipwa mishahara kinyume na utaratibu za utumishi.