Showing posts with label Mhe.Freeman Mbowe. Show all posts
Showing posts with label Mhe.Freeman Mbowe. Show all posts

Wednesday, September 28, 2016

MAHAKAMA YAKANA KUITAMBUA KAMPUNI ILIYOTUMIWA NA NHC KUMTIMUA MBOWE

Mahakama Kuu imekana kuitambua kampuni ya Fosters Auctioneers and General Traders iliyohusika kuondoa vitu vya kampuni za Freeman Mbowe kwenye jengo la Shirika la Taifa la Nyumba (NHC).

Hayo yalibainishwa jana na kiongozi wa jopo la mawakili wanaomtetea Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti wa Chadema, Peter Kibatala wakati wa usikilizwaji wa maombi yaliyofunguliwa na mlalamikaji huyo kupitia kampuni ya Mbowe Hotels Ltd dhidi ya NHC na kampuni hiyo ya udalali.

Saturday, June 11, 2016

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO WAIPELEKA SERIKALI MAHAKAMANI

MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, jana alifungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, kupinga amri ya polisi kuzuia mikutano ya vyama vya siasa nchini.