Showing posts with label Mhe. Wiliam Ole Nasha. Show all posts
Showing posts with label Mhe. Wiliam Ole Nasha. Show all posts

Tuesday, June 14, 2016

SERIKALI YAUNDA KIKOSI KAZI KUDHIBITI UVUVI HARAMU WA KUTUMIA MABOMU

Serikali imeunda kikosi kazi kwa ajili ya kushughulikia uharibifu wa kimazingira ikiwemo kudhibiti uvuvi haramu wa kutumia mabomu ili kulinda mazalia ya samaki na kulinda ikolojia ya bahari.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Wiliam Ole Nasha alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Chambani (CCM), Mhe. Yusuf Salim Hussein aliyetaka kujua hatua zinazochukuliwa na serikali kuzuia uvuvi haramu wa kutumia mabomu.