Showing posts with label Jimbo la Kijitoupele. Show all posts
Showing posts with label Jimbo la Kijitoupele. Show all posts

Saturday, March 19, 2016

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) HAITAMBUI KUJITOA KWA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KIJITOUPELE ZANZIBAR

Na Clarence Nanyaro- NEC
Tume  ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),imesema haitambui  kujitoa kwa Chama cha Wananchi (CUF),katika uchaguzi wa Mbunge  Jimbo la Kijitoupele hapa Zanzibar unaotarajiwa kufanyika Jumapili licha ya kuwa  Tume imepokea barua rasmi toka kwa uongozi wa Chama hicho.
Mkurugenzi wa uchaguzi wa Tume ya Taifa Bw Kailima Ramadhani amesema Tume imefikia maamuzi hayo kutokana na ukweli kuwa barua hiyo ya CUF imechelewa huku maandalizi ya uchaguzi huo yakiwa yamekamilika na ni Wananchi tu kwa sasa Wanasubiriwa kwenda kupiga kura.