Showing posts with label Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Show all posts
Showing posts with label Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Show all posts

Tuesday, June 21, 2016

NOAH YAACHA NJIA NA KUPARAMIA DALADALA, BUZA JIJINI DAR ES SALAAM WANAJESHI WANUSURIKA KIFO

 Wananchi wakiangalia ajali ya Noah yenye namba za usajili T 359 DFQ iliyodaiwa kuacha njia na kuparamia daladala namba T 797 DEW eneo la Buza Njia Panda ya Kitunda jijini Dar es Salaam. Katika ajali hiyo watu wawili waliokuwa kwenye Noah hiyo waliotajwa kuwa ni Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), walijeruhiwa na kukimbizwa Hospitali ya Temeke kwa matibabu.

Saturday, March 26, 2016

SIMU AINA YA TECHNO YAONDOA UHAI WA KIJANA MWENYE UMRI WA MIAKA 16 MKOANI KIGOMA:


Askari nane wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wanashikiliwa na Polisi Mkoa wa Kigona wakituhumiwa kwa mauaji ya Erick Nilamewa (16) waliyemtuhumu kuwaibia simu moja aina ya Techno na Sh. 6,000.
Tukio hilo lilitokea juzi jioni Mtaa wa Mabatini Mwanga Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Wanajeshi hao wakiwa nane, walionekana wakimpiga Nilamewa kwa mateke, fimbo na kumchoma na pasi tumboni, kifuani na mgongoni, baada ya kumkamata wakimtuhumu kwa wizi huo.
Mwili wa kijana huyo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Mkoa Maweni.
Aidha, Ahamad Mussa, mkazi wa Mabatini eneo la Mwanga Manispaa ya Kigoma/Ujiji, amelazwa wodi namba 7 katika hospitali ya Mkoa Maweni kwa matibabu, kutokana na purukushani hiyo.

Friday, March 18, 2016

UCHAGUZI ZANZIBAR: CHAMA CHA CUF KIMEWATAKA WANACHAMA NA WANANCHI WOTE KUKAA NDANI SIKU YA UPIGAJI KURA KATIKA UCHAGUZI WA MARUDIO:

Siku ya Jumapili, tarehe 20 Machi 2016, Zanzibar itashuhudia, kwa mara nyingine tena, ubakwaji wa demokrasia kwa kufanyika kile kinachoitwa Uchaguzi wa Marudio’ kufuatia tamko binafsi la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, alilolitoa tarehe 28/10/2015 kwamba ameufuta Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25/10/2015 na matokeo yake yote.