Showing posts with label Jeshi la Polisi Mkoani Arusha. Show all posts
Showing posts with label Jeshi la Polisi Mkoani Arusha. Show all posts

Friday, April 15, 2016

JESHI LA POLISI MKOANI ARUSHA, LIMEMKAMATA ISAACK HABAKUK EMILY KWA KUTUMIWA KUMTUKANA RAIS POMBE MAGUFULI:


Jeshi la Polisi Mkoani Arusha, limemkamata Isaack Habakuk Emily, kwa kosa la kumtukana Rais John Magufuli kuwa ni bwege na kwamba hawezi fananishwa na Nyerere na kusambaza ujumbe kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza ofisini kwake, leo jijini Arusha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Machi 22 mwaka huu eneo la Hotel ya Anex jijini humo.

Amesema kuwa baada ya kumkamata alifanyiwa upekuzi na kukutwa na simu ya kiganjani aina ya Tecno iliyotumika kutenda kosa la kutuma ujumbe wa kumkashifu Dkt. Magufuli.