Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Juma Aweso (wa pili toka kulia) akiwa na katibu tawala wa Wilaya ya Temeke, Edward Mpogolo wakati wakipatiwa maelezo machache juu ya uharibifu wa miundo mbinu ya maji inayofanywa na wananchi wasio waaminifu wakati wa ziara ya Naibu huyo aliyoifanya katika manispaa ya Temeke na Ilala ili kujionea miradi mbali mbali ya maji.
Tuesday, February 20, 2018
DAWASA NA DAWASCO ZATAKIWA KUPELEKA HUDUMA ZA MAJI PEMBEZONI MWA JIJI LA DAR
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Juma Aweso (wa pili toka kulia) akiwa na katibu tawala wa Wilaya ya Temeke, Edward Mpogolo wakati wakipatiwa maelezo machache juu ya uharibifu wa miundo mbinu ya maji inayofanywa na wananchi wasio waaminifu wakati wa ziara ya Naibu huyo aliyoifanya katika manispaa ya Temeke na Ilala ili kujionea miradi mbali mbali ya maji.
Wednesday, February 14, 2018
AWESO ATAKA MIRADI YA MAJI IKAMILIKE KWA WAKATI
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akikagua bomba la DAWASCO linalosambaza Maji ya Ruvu Juu iliyopo maeneo ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Saturday, February 10, 2018
SIDO YATANGAZA VITA NA WADAIWA WAKE SUGU
Meneja wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) mkoa wa Dar es Salaam Macdonald Maganga akitoa uamuzi wa wao kuwaweka kampuni ya udalali ya Yono Auction kwa ajili ya kwenda kukamata wadaiwa sugu wote.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart, Scholastica Kevela akitoa tamko la siku 14 kwa wadaiwa sugu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), kulipa madeni yao kabla ya chukuliwa hatua za kisheria ikiwamo mali zao kupigwa mnada kufidia deni.
Meneja wa SIDO mkoa wa Dar es Salaam Macdonald Maganga akiongoza wafanyakazi na viongozi wa Yono kupita mlango kwa mlango wakati wakizundua kampeni ya kudai madeni "LIPA DENI LAKO SIDO, KUWA MZALENDO'.
Wakiingia katika moja ya ofisi za mdaiwa wa SIDO.
Nae Mwenyekiti wa Kuatamia mawazo ya wabunifu, Joseph Mlay ameiunga mkono SIDO kwa hatua waliyochukua ya kuingia mlango kwa mlango katika kudai madeni yao. Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), mkoa wa Dar es Salaam imetangaza vita kwa wale wadaiwa sugu kulipa madeni yao kabla ya chukuliwa hatua za kisheria ikiwamo mali zao kupigwa mnada. Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam, Meneja wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), mkoa wa Dar es Salaam Macdonald Maganga wakati akizindua kampeni ya kukusanya madeni kwa wateja wao. "Leo tunazindua kampeni ya kukusanya madeni kwa wadaiwa sugu wote wa SIDO hatutakuwa na huruma juu ya hili maana hawa ndiyo wanarudisha maendeleo ya shirika nyuma, kuna waliokopa, walipanga kama haujalipa deni lako ujue tunakupa siku 14 tu baada ya hapo sheria itachukua mkondo wake," amesema Mkurugenzi Maganga. Meneja Macdonald Maganga amesema wadaiwa ni wale waliopewa maeneo maalumu ya viwanda kwa ajili ya kufanyia kazi zao na waliopatiwa huduma ya fedha kwa mkopo na kushindwa kurejesha kwa wakati. “Kuna ambao wamekaa miaka mingi au miezi mingi bila kurejesha fedha kwetu kama shirika inatuathiri kwa sababu hatuwezi kuwahudumia wengine,” amesema Maganga. Maganga amesema wanadai jumla ya sh. milioni 350 kutoka kwa wadaiwa zaidi ya 77. Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart, Scholastica Kevela amewashukuru SIDO kwa kuweza kuwapa kazi hiyo ya kuwakusanyia madeni na kuongeza kuwa hawata muonea huruma mdaiwa yeyote. "Yono Auction Mart tunatoa siku 14 kwa wadaiwa sugu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), kulipa madeni yao kabla ya chukuliwa hatua za kisheria ikiwamo mali zao kupigwa mnada kufidia deni,". amesema Mama Kevela. “Kwa wadaiwa wote wa SIDO, wanaoishi kwenye viwanda na nyumba za SIDO bila kulipa pango, waliochukua mikopo na hawataki kurejesha kwa sababu wanazozijua wao, mkono wa Yono uko kazini ni vyema wakachukua hatua wakalipa ili kuondosha usumbufu,” amesema Kevela.

Mdaiwa Masoud amedai hawafanyi makusudi kutolipa madeni ni kutokana na kodi kupanda kila mwaka huku hali ya biashara ikiwa mbaya.
“Ukizingitia soko la ushidani na hali ya bidhaa unashindwa kuuza kwa wakati kwa hiyo tunalipa lakini hatulipi kwa wakati,” amesema.
Amedai wamepangishwa kwa zaidi ya miaka 40 wakifanya shughuli zao na kama wangekuwa hawalipi kwa kipindi chote wangefukuzwa hivyo ameiomba serikali kutodhani kuwa wanapuuza kulipa madeni.
Friday, February 09, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ameongoza mamia ya wananchi katika mazishi ya Mzee Kingunge Ngombale Mwiru ambayo yamefanyika katika makaburi ya Kinondoni leo Jumatatu Februari 05, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamini Wiliam Mkapa pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakiwa katika ibada ya mwisho ya marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamini Wiliam Mkapa pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakishuhudia mwili wa marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru ukishushwa kaburini katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka mchanga kwenye Kaburi la marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamini Wiliam Mkapa pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuweka udogo kwenye kaburi la marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijiandaa kuweka Shada la Maua kwenye Kaburi la Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka Shada la Maua kwenye Kaburi la Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali mara baada ya kuweka Shada la Maua kwenye Kaburi la Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na waombolezaji mara baada ya maziko ya marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Thursday, February 01, 2018
UCHUMI WA TANZANIA YATAKIWA KUJENGWA NA WAJASILIAMALI
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathow Mmuni ambaye alikuwa mgeni rasmi akifunga mfunzo ya wajasiliamali yaliyoendeshwa na Sido mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Mkurugenzi wa Sido Dar es Salaam, MacDonald Maganga.
Subscribe to:
Posts (Atom)