Showing posts with label vibanda 35 na maduka matano.. Show all posts
Showing posts with label vibanda 35 na maduka matano.. Show all posts

Tuesday, April 12, 2016

MOTO WATEKETEZA SOKO KARAGWE MKOANI KAGERA USIKU WA KUAMKIA:

Na Amos Petro Kagera
Moto mkubwa umezuka na kuteketeza soko la mji wa Kayanga wilaya ya Karagwe mkoani Kagera usiku wa kuamkia leo. 

Moto huo ambao unadaiwa kuwa ulianza majira ya saa 2 ya usiku wa jana umeteketeza vibanda 35  na maduka matano.

Wafanyabiashara wengi katika soko hilo wamesikitishwa na kutokea kwa janga hilo, kwani wengi wao wamesema walikuwa na mikopo na hawakuwa na bima ya mali zao.

Jonasi Nyarugenda ni miongoni mwa wafanyabiashara hao anasema “Moto umeteketeza stoo zangu nne zenye bidhaa mbalimbali kama sukari, mchele, ngano na mafuta, kwakeli ukitathimini kwa haraka siyo chini ya milioni 45 zimepotea.”