Showing posts with label mwanamke Oliver Erasto. Show all posts
Showing posts with label mwanamke Oliver Erasto. Show all posts

Friday, May 06, 2016

TAMKO LA WIZARA KULAANI MAUAJI YA MAMA NA MTOTO, B/MOYO

































Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto inasikitishwa na inalaani vikali tukio la kuuawa kwa kuchinjwa, mwanamke Oliver Erasto (23) na mtoto wake Emmanuel (3), wakazi wa eneo la Zinga, kata ya Dunda, wilayani Bagamoyo, kutokana na wivu wa kimapenzi.

Wizara inakemea maauji hayo, yanayodaiwa kutekelezwa na Frowin Mbwale mkazi wa Kawe, Dar es salaam, ambaye ni mme wa marehemu, kwani yamesababisha kukatisha maisha ya mama na mtoto, katika kipindi ambacho Taifa linahimiza uzingatiaji wa mchango na haki za wanawake katika maendeleo ya taifa, na mwitikio wa haki ya kuishi ya Mtoto katika mipango na programu za maendeleo endelevu.