Showing posts with label Vayalet Michael.. Show all posts
Showing posts with label Vayalet Michael.. Show all posts

Sunday, April 17, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI MOROGORO:

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimfariji Bibi Fausta Andreas na Mtoto wake Vayalet Michael (2) aliyelazwa katika Hospitali ya rufaa Mkoa Morogoro kwa matibabu wakati alipotembelea Hospitali hiyo April 17.2016 kwa ajili ya kuangalia utendaji na utoaji huduma kwa Jamii. Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
mo2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimfariji Mtoto Anisha Juma (2) mkazi wa Morogoro mjini aliyelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro kwa matibabu leo April 17.2016 Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro kwa ajili ya kuangalia utendaji kazi na utoaji huduma kwa Jamii.