Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya NMB Kitengo cha Hazina wakimkabidhi mashine ya kumsaidia mtoto anayeshindwa kupumua vizuri (Suction Machine) Ichaji wa Wodi 'A' ya Watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili, Sista Devota Ndendeje (mwenye nguo nyeupe) walipotembelea wagonjwa waliolazwa katika Wodi ya Watoto Hospitalini hapo juzi. Vifaa vingine vilivyokabidhiwa ni ENT Seti mbili kwa ajili ya vipimo vya masikio, koo na pua kwa watoto, mashine ya kuwasaidia watoto wenye pumu (Nebulizer machine), Digital thermometer 14, pampers, sabuni, mafuta ya vaseline, cotton buds, miswaki na dawa za miswaki, toilet papers, chupa za maziwa kwa watoto wachanga na zawadi nyingine kwa watoto kama pipi, juice, biscuits na chama.