Showing posts with label Shirika la Misaada la Korea (KOICA). Show all posts
Showing posts with label Shirika la Misaada la Korea (KOICA). Show all posts

Tuesday, June 14, 2016

UJENZI WA HOSPITALI YA KISASA CHANIKA KUGHARIMU BILIONI 18













Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Shirika la Misaada la Korea (KOICA) inatarajia kutumia kiasi cha shilingi bilioni 18 kukamilisha Ujenzi wa Hospitali ya kisasa ya kutolea huduma za matibabu kwa mama na mtoto katika Kata ya Chanika,wilayani Ilala.

Hayo yamesemwa  Jijini Dar es Salaam na Afisa Habari wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, David Langa wakati akitoa ufafanuzi kuhusu maboresho yanayofanywa katika Sekta ya Afya ndani ya Manispaa hiyo.