Showing posts with label Msemaji Wa Jeshi la Polisi Advera Bulimba.. Show all posts
Showing posts with label Msemaji Wa Jeshi la Polisi Advera Bulimba.. Show all posts

Thursday, April 14, 2016

JESHI LA POLISI LAWATAADHARISHA WATANZANIA KUHUSU UTAPELI WA AJIRA KATIKA TAASISI MBALIMBALI:

Msemaji Wa Jeshi la Polisi Advera Bulimba.
Katika siku za hivi karibuni katika maeneo mbalimbali hapa nchini, kumejitokeza makundi ya watu ama mtu binafsi kutumia mwamvuri wa taasisi fulani kujipatia kipato kwa njia za udanganyifu (utapeli) kwa kuwaahidi vijana kwamba watawapatia ajira katika taasisi hizo.

Makundi haya ya kihalifu imebainika kwamba yapo katika maeneo mbalimbali, hivyo, ni suala ambalo linahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi ili kukomesha vitendo hivyo.