Showing posts with label Mhe. Salva Kiir Mayardit. Show all posts
Showing posts with label Mhe. Salva Kiir Mayardit. Show all posts

Friday, April 15, 2016

RAIS WA SUDANI KUSINI, MHE. JENERALI SALVA KIIR MAYARDIT AWASILI NCHINI NA KUSAINI MAKUBALIANO YA KUJIUNGA NA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.

Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye kofia nyeusi) akishuka katika ndege ya Shirika la Kenya mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Thursday, April 14, 2016

ZIARA YA MHE. SALVA KIIR, RAIS WA JAMHURI YA SUDAN KUSINI TANZANIA TAREHE 15 APRILI 2016:


Ziara ya Mhe. Salva Kiir, Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Tarehe 15 Aprili 2016.
 
Mhe. Salva Kiir Mayardit, Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini atafanya ziara ya kikazi ya siku moja nchini Tanzania tarehe 15 Aprili 2016. 

Rais Kiir anakuja nchini kusaini Mkataba wa kuwezesha Jamhuri ya Sudan Kusini kuwa Mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambapo tangazo la kukubaliwa kuwa Mwanachama wa EAC lilitangazwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa EAC uliofanyika jijini Arusha mwezi Machi 2016.